Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na ujenzi wa Jengo la kisasa la ghorofa moja la Halmashauri ya wilaya ya Mbinga ambalo limejengwa kwa shilingi bilioni 3.3 hadi kukamilika kwake.
Alisema kuwa anawashukuru amefika Mbinga kwa madhumuni ya kufungua jengo na amewapongeza halmashauri hiyo kwa kukamilisha ujenzi huu wa jengo hilo zuri .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hayo ameyasema wakati akifungua jengo la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga mkoani Ruvuma.
Akizundua jengo hilo amesema kukamilika kwa jengo hilo ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukamilika jengo hilo wahakikishie huduma zote zinatolewa ndani ya nyumba moja .
“Ni jengo zuri nimeingia ndani kuangalia ujenzi unaridhisha sana na ni jengo lenye nafasi za kutosha kwa hiyo nawashukuru sana lakini pamoja na hilo niwapongeze madiwani kwamba mmesimamia ujenzi wa jengo hili lakini pia mmewaza kuwa na jengo la kitega uchumi jengo la kuwawezesha wananchi nimuombe Mungu awatie nguvu na mlimalize jengo hilo liweze kufanya kazi iliyokusudiwa” alisema Rais Samia.
Alisema kuwa kukamilika kwa jengo hilo ni kukuwa kwa utawala bora maofisi yote wakiwemo wakuu wa idara na kila mtu yumo humo ndani kwa maana hiyo huduma zote zitatolewa ndani ya nyumba moja ili kuharakisha huduma kwa wananchi lakini pia kuleta utawala bora ili haki za wananchi zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo .
” Niwasisitize watakaotumia nyumba hii madhumuni ya serikali kujenga nyumba hizi ni kuleta mazingira mazuri kwa maafisa wetu wanafanya kazi ndani ya halmashauri hizi ni kurahisisha utendaji wa kazi kwa hiyo niwaombe sana maofisa wote kutumika Majengo haya kwa kutulia na kufanya kazi zao vizuri kwa kuhudumia wanachi kwa upendo na weledizaidi.”alisema Rais Samia.
Naye Mbunge jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga amesema,Wanamshukuru kwa miradi mingi aliyopeleka kwenye jimbo hilo wamepata miradi ya maji bilioni 13.9 , Barabara-Amani Makolo-Mbambabay bilioni 60 elimu bilioni 10 afya bilioni 2.2 ujenzi wa vituo vya Afya bilioni 836 na bilioni 2.8 upande wa Barabara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.