MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekagua ujenzi wa miradi ya maabara na huduma za afya inayotekelezwa katika Kata za Luchili,Mkongp gulioni na Ligera wilayani Namtumbo ambapo ameagiza wananchi kushirikishwa kikamilifu katika hatua zote za utekelezaji wa miradi hiyo.
Rc Ibuge pia ameagiza taraitibu zote za kifedha kuzingatiwa kwenye miradi hiyo pamoja na kufuata miongozo ya serikali na kuhakikisha fedha zinatumika kulingana na thamani ya mradi. ambapo ameagiza usimamizi wa miradi na kuunda kamati kulingana na mahitaji ya miongozo.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amekagua shule nne za sekondari kati ya saba ambazo serikali imetoa shilingi milioni 210 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ambapo kila sekondari imepewa shilingi milioni 30.Sekondari zilizokaguliwa ni Luchili,Lukwimwa,Kimoro na Nahimba.
RC Ibuge pia amekagua ujenzi wa zahanati ya Misufini Kata ya Luchili ambayo seriikali imetoa shilingi milioni 50 pia amekagua mradi wa ujenzi wa vyoo katika kituo cha afya Mkongo gulioni unaogharimu shilingi milioni 35.
Tazama habari zaidi hapa https://www.youtube.com/watch?v=fkAGkSlpZ_k&t=88s
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.