MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa Mazingira Songea unatarajia kukamirisha mradi wa maji unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 500.
Akitoa taarifa hiyo Mhandisi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Frenk Tamsi amesema mradi huo umejengwa katika mtaa wa pambazuko ,mlete pamoja na chuo cha uhasibu Arusha Tawi la Songea Manispaa ya Songea na kuhudumia wananchi wapatao 3,900.
Tamsi amesema mradi huo unafadhiliwa na Wizara ya Maji kupitia mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19 na unatarajia kukamilika Juni 28,2022.
Amesema mradi huo unajengwa na mkandarasi Jambela Limited kwa mda miezi sita ikiwa na vyanzo vya maji visima viwili vyenye uwezo wa kuzalisha lita 518,400 kwa siku na utekelezaji huo umefikia asilimia 70.
“Mamlaka inasimamia mradi kwa kutumia wataalamu wake wa ndani ili kuhakikisha kazi inatekelezwa kwa ubora,usalama na kwamda uliopangwa”.
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumza mara baada ya kupokea taarifa amemwagiza Mkandarasi wa Mradi wa Maji Mtaa wa Pambazuko kuhakikisha anamaliza kazi yake ndani ya Mkataba.
Ibuge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za mradi huo kwa asilimia 100 ikiwa ni utekeleza wa ilani ya CCM.
Moja kati ya wanawake wa mtaa wa pambazuko Mariam Mpoma amepongeza jitihada za Serikali katika kusaidia kumtua mama ndoo kichwani ikiwa wakati wa awali wanapata maji kutoka kwenye mito ambayo siyo salama kwa afya.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Habari Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Juni 1,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.