Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka watu wote wanaotumiwa kuhujumu vifaa vya Kampuni ya CHICCO inayojenga barabara ya Mbinga hadi Mbambabay.
Mndeme ametoa maagizo yao baada yakupata taarifa kutoka kwa uongozi wa kampuni ya CHICCO kuwa kuna watu wameiba vifaa vya mitambo inayitumika kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami nzito yenye urefu wa kilometa 67.
Mndeme amesikitishwa kitende cha Wizi wa vifaa vya kutengenezea Barabara hiyo ambayo serikali imetoa shilingi bilioni 129 kutekeleza mradi huo ambao unatarajia kukamilika mwaka huu.
Utekelezaji wa mradi huu hadi sasa ni zaidi ya asilimia 50 ambapo Mndeme amesema Serikali imeamua kuwaondolea kero wananchi wa Mbinga na Nyasa waliokuwa na kiu ya kuona Barabara inakuwa kwa kiwango cha Lami lakini watu wachache wanataka kupoteza furaha yao kwa kuiba vifaa.
Mkuu wa Mkoa amemesikitishwa na kampuni iliyopewa dhamana ya Kulinda vifaa hivyo ambapo ameagiza wahusika wote wakamatwe na wachukuliwe hatua ya kisheria dhidi yao, na mkataba na kampuni inayolinda uvunjwe.
,,Mimi niseme Ndugu zangu Chicco nimeumia sana na nimesikitika sana sikutegemea kama kampuni iliyopewa dhamana ya ulinzi huu ambao mmeingia nao mkataba wao wanakuwa wa kwanza kutuibia sasa mimi niwaahidi tu naenda kuchuwa hatua kuanzia sasa hawa wote waliofanya wizi huu tutawakamata’’.alissisitiza Mndeme
Mndeme ameitaka kampuni hiyo iliyoiba vifaa kama wanamadai yao wafuate taratibu kwa sababu kwa wizi uliofanyika wamesababisha baadhi ya mitambo ya kampuni ya Chicco imesimama haifanyi kazi jambo ambalo halikubaliki.
Mkuu wa Mkoa amewaagiza Kampuni ya Chicco kuendelea na mradi huo kwa kununua betri na Mafuta ili kazi ziendelee.
Kampuni ya CHICCO katika Mkoa wa Ruvuma inasimamia miradi minne ikiwemo mradi wa Barabara Mbinga Mbambabay, ujenzi wa Bandari ya Ndumbi,Uwanja wa Ndege wa Songea na Mradi wa barabara ya Kitai hadi Amani Makoro.
Mwakilishi wa Kampuni ya CHICCO alivitaja vifaa vilivyoibiwa kuwa ni mafuta ya petroli lita 100 betri 4 za mitambo ambapo wezi walinadika karatasi ambayo imeleza kuwa wamefanywa hivyo ili walipwe fidia zao.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Mbinga
Juni 24,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.