MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amezindua Mradi mkubwa Wa Maji Katika Kijiji cha mkowela kata ya namakambale, Mradi Huo umejengwa kwa fedha za ndani zilizotolewa na serikali kuu kupitia RUWASA, Akizindua mradi huo Mkuu wa mkoa amewataka wananchi kuutunza ili uendelee kuleta manufaa endelevu, aidha amewapongeza viongozi na wafanyakazi wa RUWASA kwa kusimamia kiuadilifu fedha za mradi huo ambao ulitengewa T.sh 160 milioni, na wao wameweza kukamilisha mradi huo kwa T.sh 131 milioni tu! Na kubakiwa na Milioni 29.
Pia mkuu wa mkoa amewapongeza wanachi hao kwa kuendelea kuwa na imani na chama cha mapinduzi kwa kupigia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kwani mradi huo ni matunda ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
Akitoa shukrani kwa serikali diwani wa kata ya nambakambale Mhe.Wadali, ameahidi kushirikiana na wananchi hao katika miradi mingine kwenye kata yake
Habari imeandikwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.