Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameendelea na ziara yake ya kukagua migodi ya madini mkoani Ruvuma inayotekelezwa katika wilaya mbalimbali ikiwemo wilaya ya Mbinga,Namtumbo,Tunduru,Songea na Nyasa.
Hadi sasa amekagua miradi katika wiaya za Namtumbo na Mbinga ,akiwa katika wilaya ya Mbinga ametembelea Kampuni ya uchimbaji makaa ya mawe ya Jitegemee Holdings,ambayo inamiliki mgodi wa Makaa ya mawe katika kijiji cha Ntunduwaro Kata ya Ruanda Wilaya ya Mbinga.
Shughuli za uzalishaji katika mgodi huo zilianza rasmi Mei 2021 na mgodi una uwezo wa kuzalisha tani 2,500 hadi 3,000 za makaa ya mawe kwa siku kwa mashine zilizopo kwa sasa.
Hata hivyo hadi kufikia Desemba 2022, jumla ya dani 652,128.8 za makaa ya mawe zimevunwa.Hadi kufikia Desemba 2022 kampuni ilikuwa imeuza jumla ya tani 522,450.08 za makaa ya mawe kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.