Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amewasisitiza wazalishaji wa makaa ya mawe kuongeza kasi ya uzalishaji ili kuongeza pato la taifa.
Ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake katika sekta ya madini ambapo ametembelea migodi ya makaa ya mawe iliyopo Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, ziara hiyo imehusisha mgodi wa RUVUMA COAL, TANCOAL, MILCOAL na JITEGEMEE.
“Biashara hii ni ya kifursa, vita ya Urusi na Ukraine imeleta uhitaji mkubwa wa umeme kutoka kwenye makaa ya mawe, hapa nipo kuwasisitiza wazalishaji wa makaa ya mawe ndani ya mkoa wetu kuongeza kasi ya uzalishaji, usafirishaji na uuzaji nje katika kipindi hiki cha mpito ambapo bado mazungumzo ya kusitisha vita yanaendelea kufanyika,” alisema Kanali Ahmed.
Amewataka wanapoendelea kufanya uzalishaji wa makaa ya mawe kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kuwa maeneo yenye uzalishaji mkubwa huwa na uchafuzi wa mazingira.
Akitoa taarifa ya mgodi wa TANCOAL, Meneja Uzalishaji wa Kampuni hiyo, Mhandisi Enock Mwambeleke, amesema kampuni hiyo imekusudia kuongeza uzalishaji wa makaa hayo kutoka tani 25,000 hadi kufikia tani 100,000 kwa mwezi mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.