MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas ametembelea hifadhi ya Milima ya Matogoro.
Thomas katika ziara hiyo amekagua mlango wa kuingilia uliogharimu zaidi ya Shilingi 200.
Mkuu wa Mkoa amesema wananchi ni sehemu ya uhifadhi hivyo wasichome moto misitu ni urithi.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeth Mgema amesema hifadhi ya milima ya Matogoro ni ya mda mrefu na haijawahi kuwa chanzo cha mapato kwasababu haikuboresshwa.
Amesema ujenzi wa Mlango wa Kuingilia pamoja na Barabara utasababisha kufikika mpaka Juu pamoja na kuongeza thamani ya Hifadhi.
Mgema ameishukuru Serikali kwa kuleta fedha alizotoa shilingi milioni 200 ya kuongeza thamani ya hifadhi ya Milima ya Matogoro.
“Tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuletea fedha ambayo imesababisha kuongeza thamani ya hifadhi”.
Amesema Majira wa milima hiyo wanafanya shughuli mbalimbali za kijamii zinasababisha athari ya hifadhi ikiwemo kilimo ikiwa kisheria wanakwenda mpaka kwenye kingo cha mto wanasababisha kukausha vyanzo vya Maji.
Mgema ametoa rai kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo watambue kuwa hifadhi ya Mlima ya Matogoro ni yao na inasababisha kuhudumia Wilaya ya Songea katika Swala nzima la Maji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 12,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.