MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka wazazi mkoani Ruvuma kuwajibika ipasavyo katika malezi ya watoto wao
Hayo ameyasema wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambapo amewataka na amewahiza kushiriki katika Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi wa wanawake na watoto.
Kanali Thomas amesema wazazi wajenge tabia ya kuzungumza na watoto wao kila mara kwani malezi bora kwa watoto utokana na wazazi hivyo ni vyema wazazi wapate muda kuwasikiliza ili wajue changamoto wanazopitia
“Tujitokeze tuungane na wezetu katika kuhamasisha na kukemea ukatili dhidi ya watoto na asa watoto wadogo muandae muundo wa kupita katika mashule kuongea na wa walimu pamoja na wanafunzi kwani uko ndipo watoto zetu ukutana tabia tofauti” amesema Kanali Thomas
Kampeni hii hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.