Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amezindua minada ya zao la korosho kwa Mkoa wa Ruvuma.
Uzinduzi huo umefanyika katika kata ya Nakapanya ,Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na kuhudhuriwa na wataalam, wadau pamoja na wakulima wa za hilo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuboresha sekta ya Kilimo.
"Niendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya haswa kwenye Sekta ya Kilimo, sisi Mkoa wa Ruvuma tukiwa ni wanufaika wakubwa wa sekta hiyo", Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred amebainisha kuwa bei zinazoendelea wakati huu katika Minada ndiyo bei zilizopo katika mwenendo wa Soko la Dunia.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa Bodi ya Korosho ilitarajia mwenendo wa bei ya Korosho kwenye Soko la Dunia kuwa kati ya 3,000 Hadi 3,600 na ikizidi sana ni hadi 3,800.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Chacha ameishukuru Serikali kwa kuweka jitihada kubwa za kuwasaidia Wananchi kwa kutoa Pembejeo kwa kiwango kikubwa.
Msimu wa 2024/2025 Mkoa wa Ruvuma umekusudia kuzalisha na kuuza korosho Tani 28,000 sawa na kilo 28,0000,000.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.