MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa wito kwa wakandarasi wa mradi wa utekelezaji wa umeme wa Rea kumaliza kazi kwa mda waliopangiwa.
Hayo amesema ofisini kwake alipotembelewa na wataalamu kutoka Bodi ya Nishati vijijini (REA) na Bodi ya Nishashati vijijini (REB) Dodoma.
Ibuge amesema wakandarasi kabla ya kuanza kazi wapeleke mpango kazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na kuwajulisha wananchi katika maeneo waliyopo mda wa kufanya kazi na kumaliza ili wajue mda wa utekelezaji wa kazi hiyo na kukamilika.
“Wakandarasi wanapoanza utekelezaji walete mpango kazi Mkoani ili mda uliopangwa usibadilishwe katika utekelezaji na kukimbizana na maeneo ambayo kipindi cha mvua hayawezi kupitika itapelekea kuepuka changamoto ya barabara”.
Wakili Julius Kalolo Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati vijijini (REB) amesema baada ya kupata malalamiko kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamekuja na kujionea kuwa mkandarasi bado hana mwelekeo wa kumaliza kazi kwa wakati ikiwa mradi ulianza Juni 15,2018 ulitakiwa kumalizika mwaka jana Juni 14,2020.
Kalolo amesema baada ya kufanya utafiti walimuongezea baadhi ya vijiji lakini haikuwa sababu ya kuchelewa lakini bado kuna maeneo ambayo asiweze kujenga miundo mbinu na kupeleka vifaa baadhi ya maeneo kwasababau kipindi cha mvua kinakaribia.
“Mkandarasi na Namesi anasingizia amepewa eneo kubwa lakini je eneo dogo alilofanya kazi ni lipi ilikuonyesha pamoja na ukubwa “.
Kwaupande wake Mhandisi Hassan Saidy Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA) amesema wandarasi pamoja na wafanyakazi wao wanapokuwa kazini wahakikishe wanakuwa na nidhamu na hawafanyi vitendo visivyofaa kwa kuongea maneno machafu pamoja na kuchukua rushwa.
Amesema mkandarasi analeta vifaa vyenye ubora na kama havitakuwa na ubora atarudishiwa kwa gharama zake za kurudisha na kuleta vifaa vyenye ubora,pamoja na kutunza vifaa katika mazingira mazuri na wanapokuwa katika eneo la kazi inawapasa kulipoti kwa Mbunge,diwani,mtendaji na Mwenyekiti wa kijiji ili wananchi wajue kinachoendelea katika eneo hilo.
Imeandikwa na Aneth Ndonde
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.