MKOA wa Ruvuma umetekeleza miradi ya EP4R awamu ya 9 na ujenzi wa Vyoo vya kisasa kwa bajeti ya mwaka 2020/2021.
Akizungumza Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Hakimu Mafuru Ofisini kwake amesema Serikali katika kuhakikisha inapunguza Changamoto za Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari hadi kufikia octoba 2020 Mkoa ulipokea zaidi ya Shilingi bilioni 6 kupitia mradi wa EP4R awamu ya 8.
Mafuru amesema kati ya fedha hizo kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 700 kwaajili ya ukarabati wa Shule kongwe ya Tunduru Sekondari.
Amesema Miundombinu mingine iliyojengwa ni ujenzi wa vyumba vya Madarasa matundu ya vyoo,mabweni,mabwalo na majengo ya utawala.
Hata hivyo amesema pamoja na utekelezaji wa miradi hiyo Mkoa ulipokea zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka Serikalini kwaajili ya Ujenzi wa Vyoo bora vya kisasa vya wanafunzi na walimu kupitia mradi wa SWASH(Shool water,sanitation and Hygiene) ambapo jumla ya vyoo 60 vyenye matundu 800 vimejengwa.
Afisa Elimu amesema kwa mwaka wa fedha 2019/2021 Mkoa kupitiia Halmashauri zake umepokea kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni sita kutoka hazina kwaajili ya ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya Madarasa ujenzi wa matundu ya vyoo pamoja na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa Shule za Sekondari na Msingi.
Amesema Sera ya utoaji wa Elimu bila malipo inaendelea kutekelezwa ambapo kwa kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Novemba 2021 Mkoa umepokea kiasi cha zaidi ya ya shilingi bilioni 2 zimesaidia katika uendeshaji wa Shule na kuboresha na kuimarisha ufundishaji.
“Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri zake unaendelea kufuatilia na kutekeleza kwa ufanisi utoaji wa Elimu bila malipo ili fedha ya Serikali inayowekezwa iweze kutoa matokeao chanya katika kuongeza ufaulu wa wanafunzi”.
Mafuru amesema Mkoa umekuwa ukishirikiana na wadau mbalimbali katika kusukuma gurudumu la la maendeleo ya Elimu,katika kusaidia na uboreshaji wa mazingira ya ujifunzaji na kufundishia.
Amesema Mkoa unatambua jitihada za wadau kwa mwaka 2020/2021 wametoa zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu,huduma ya chakula Shuleni,vifaa vya TEHAMA .
“Mkoa unatambua asasi na mashirika kama vile Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),Benki ya NMB,Tanzania Project,Kalamu Education Foundation,Sociol Action Trust Fund(SATF),Tanzania Mssion to the poor and Disable(PADI),Research Triangle Institute(RTI)”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 13,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.