• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

Ruvuma yatoa washidi wawili wa NMB Bonge la Mpango

Imewekwa kuanzia tarehe: March 10th, 2022

MSHINDI wa  kampeni ya NMB Bonge la mpango tumerudi tena wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma amekabidhiwa zawadi yake ya pikipiki miguu mitatu a kwenye hafla iliyofanyika mjini Mbinga.

Mkoa wa Ruvuma umetoa washindi wawili wa pikipiki za miguu mitatu ambazo NMB kwa nchi nzima imetoa pikipiki 50.

Mshindi wa Mbinga ni Aikamesia kuro na mshindi wa Songea Ahmed Dani.

Akizungumza kwenye hafla hiyo mgeni rasmi Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amesema Kanda ya Kusini ina matawi 20 ya NMB liliwemo tawi la Mbinga.

Amesema NMB ilizindua kampeni ya NMB Bonge la mpango mwaka jana lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi kufungua akaunti na kujiwekea akiba zao wenyewe.

“Wataalam wanashauri kipato chochote unachokipata ni vema kutenga  kwenye makundi matatu,kiasi kuweke akiba ambayo itakusaidia kesho,kiasi cha pesa kutenga kwenye matumizi yako na kiasi kuwekeza kwenye shughuli inayoifanya ili iwe endelevu’’,alisisitiza Shango.

Amesema NMB inatoa elimu ya wananchi kujenga utamaduni wa kuweka akiba ambapo hivi sasa watalaam wa NMB wanapita katika shule za msingi na sekondari kutoa elimu hiyo ili kuwawezesha watoto hao kuwa na tabia ya kuweka akiba,matumizi na kuwekeza tangu wakiwa wadogo.

Meneja huyo wa Kanda NMB ameitaja Benki hiyo kuwa ina akaunti mbalimbali ambazo zitamsaidia mteja kuweka akiba na kutumia vizuri pesa zake kulingana na  anachokipata.

Shango amesema Oktoba 2022 NMB ilizindua kampeni ya NMB Bonge la mpango kuhamasisha wateja kuweka akiba walau kuanzia shilingi 100,000 hivyo kuingia moja kwa moja kwenye droo.

Hata hivyo amesema wananchi wengi waliingia kwenye droo hiyo ambapo NMB ilikuwa inashindanisha Zaidi ya shilingi milioni 300 na kushindanisha pikipiki za miguu mitatu 50 na kwamba kwenue droo hiyo NMB ilikuwa inatoa shilingi 200,000 kila wiki.

Kwa upande wake Meneja wa NMB Tawi la Mbinga Enhard Tambo amewahamasisha wananchi wa Mbinga kuendelea kufungua akaunti NMB  kupitia mawakala Zaidi ya 100 waliopo maeneo mbalimbali katika wilaya ya Mbinga ili kuingia kwenye droo ya kampeni ya Bonge la mpango.

Amesema kampeni hiyo inamwezesha mtu yeyote kushinda awe mkulima,mfanyakazi au mjasirimali na kwamba mshindi wa Mbinga alikuwa anafanya miamala ya kawaida.

Kwa upande wake mshindi wa pikipiki hiyo Aikamesia Kuro ameishukuru Benki ya NMB kwa kumpatia zawadi hiyo ambayo amesema itamsaidia katika katika biashara yake duka la spea ambapo sasa ataweza kuwapelekea wateja wake mizigo hadi nyumbani kwao.

 NMB ni Benki salama,kwa miaka tisa mfululizo  imeendelea kuongoza kwa ubora nchini Tanzania.

Imeandikwa na Albano Midelo,Ruvuma

Machi 10,2022

.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.