Mkoa wa Ruvuma umefumguka kupitia usafiri wa anga ambao umekuwa chachu katika kuleta fursa mbalimbali za maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Serikali kupitia Shirika la Ndege(ATCL) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetoa kiasi cha fedha bilioni 37 kwa ajili ya ukarabati kiwanja cha ndege kilichopo Manispaa ya Songea.
Amesema fedha hizo zimetumika katika ukarabati na upanuzi wa barabara ya kurukia ndege kutoka mita 1600 hadi mita 1860, ujenzi wa jengo la kuongozea ndege (control Tower),taa za kuongozea ndege na uzio wa usalama.
Hata hivyo amelitaja lengo kuu la Serikali kuwa kuwezesha uhakika wa usafiri wa anga utakao kuwa wa kisasa iwenye uwezo wa kutua ndege kubwa ya abiria wengi kwa mara moja .
Amesema kukamilika kwa uwanja huo kutaleta hamasa za uwekezaji pamoja na kutangaza vivutio vya utalii mbalimbali vilivyopo Mkoani Ruvuma ikiwemo Makumbusho ya Taifa ya Majimaji,ziwa Nyasa,Mto Ruvuma,Bustani ya Ruhila na vivutio vingine.
Kiwanja cha ndege cha Songea kipo daraja la tatu ambacho kinatoa huduma ya usafiri wa anga mara tatu kwa wiki kati ya Songea na Dar – es salaam ambao unafanywa kupitia ATCL.
Amesema utekelezaji wa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na Mkandarasi yupo kwenye kipindi cha uangalizi wa mradi kabla ya kukabidhi rasmi serikalini.
Kiwanja hicho ni mojawapo ya viwanja vya ndege 58 vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa niaba ya Serikali.Kiwanja cha Ndege Songea kilijengwa mwaka 1974 hadi 1980 kikiwa ambacho kiliwezesha kutua na kurukia ndege kwa kiwango cha changarawe.
Imeandikwa na Farida Baruti kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.