Ujenzi wa mabweni na madarasa katika shule za sekondari wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, umeendelea kupewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Sita kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imepokea zaidi ya shilingi milioni 826 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule mbalimbali za sekondari wilayani humo. Shule zilizonufaika ni pamoja na Sekondari za Nandembo, Tunduru, Masonya, Mataka, Matemanga, na Tarajali katika kata za Mbati na Ngapa .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Ndg. Chiza Marando, amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi hii kwa wakati na kwa ubora
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeendelea kusimamia miradi hii kwa karibu, ikiwemo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda sambamba na malengo yaliyowekwa. Pia, ushirikiano kati ya serikali, wazazi, na wadau mbalimbali umeonekana kuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha miradi hii ya maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.