Naibu Waziri Kilimo, Mheshimia Antony Mavunde, amefungua msimu wa ununuzi wa zao la korosho kwa mwaka 2022 hadi 2023 jana septemba 8 katika ukumbi wa bombambili Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano na bodi ya wadau wa korosho nchini, alisema ufunguzi wa ununuzi wa korosho kwa msimu wa mwaka 22/23 rasmi umefunguliwa na minada ya mauzo ya korosho inatarajia kuanza oktoba 14 mwaka huu
Mavunde Alisema serikali inahamasisha wadau wote wanao jihusisha na zao la korosho nchini kuzingatia miongozo na maelekezo mbalimbali iliyotolewa kwa msimu wa mwaka 2022 hadi 2023 ambao ni mwongozo wa usimamizi wa masoko na mauzo ya korosho ghafi
“Mifumo yote amabayo itawezesha kukuwa kwa zao hili tutahakisha inafanya kazi vizuri ili wakulima katika msimu huu basi watape masoko yalio ya uhakika, lengo letu serikali kuona kupitia zao la korosho tunaweza kumuinua mkulima asa kutokomeza umasikini na kutengeneza nafasi ya ajira”alisema Mavunde.
Hata hivyo amewasisitiza wananuzi na wauzaji na wadau wote wa tasnia ya korosho kufuata mfumo wa stakabadhi ghali kwa kuuza na kununu korosho kwajili ya kusafirisha nje ya nvhi pamoja na soko la awali kwaajili ya wabanguaji wa ndani
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.