Serikali inatarajia kuanza Ujenzi wa Barabara ya lami kutoka Rwanda- Lituhi Hadi bandari ya ndumbi Wilayani Nyasa.
MKuu wa Wilaya ya Nyasa mh.Filberto Sanga ameyasema hayo katika mikutano ya Hadhara iliyofanyika, kata ya Linga na Lituhi Wilayani hapa.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa Ujenzi wa Barabara hiyo,ili iweze kwenda Kasi na kukumilika Kwa Ujenzi.
"Ndugu wananchi hivi karibuni Serikali inategemea kuanza Ujenzi itakayopita katika kata zenu hivyo nichukue fursa hii kuwaombeni kutoa ushirikiano wakati wa Ujenzi wa Barabara Kwa watakaokuwa wanajenga,Kwa kuwa kukamilika Kwa Barabara hii ni fursa kubwa kwenu wananchi kukuza uchumi wenu.
Aidha ameongeza kuwa Serikali inaendelea kufanya upembuzi yakinifu katika Barabara ya Ndumbi Mbamba bay Hadi Chiwindi.
MKuu wa Wilaya ya Nyasa alikuwa katika mkutano huo kuwaeleza wananchi kazi zinazofanywa na Serikali na kusikiliza na kutatua kero Za wananchi.
Kwa upande wao wananchi wameipongeza Serikali Kwa miradi inayotekelezwa na Serikali ambayo imetatua kero za wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.