Wananchi wa Kata ya Muungano iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wametoa eneo lenye ukubwa wa ekari 9.5 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ambayo utekelezaji wake upo mbioni kuanza baada ya Halmashauri kupokea zaidi ya Shilingi bilioni 1.77 kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya Kata ya nyoni, Litembo, Muungano na nyumba ya mwalimu Kata ya Kitumbalomo.
Hayo yamebanishwa na Diwani wa Kata ya Muungano Mhe. Paulo Kayombo alipozungumza katika kikao cha kutambulisha mradi wa ujenzi wa shule hiyo kwa wananchi wa Kata hiyo kilichofanyika hivi karibuni..
“Sisi wananchi wa Kata hii tumetoa eneo ukubwa wa ekari 9.5 kudhihirisha kuwa tupo tayari kushirikiana na Serikali katika ujenzi huu,sambamba na eneo hili tutashirikiana na Serikali bega kwa bega kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati na katika ubora” Amebainisha Mhe. Kayombo
Naye Diwani wa Kata ya Kitumbalomo Mhe. Denis Kapinga amebainisha kuwa wananchi wa Kata ya Kitumbalomo wameukubali mradi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu ambayo utagharimu shilingi milioni 95 hadi kukamilika kwa kuwa mradi huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.