Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF imetoa kiasi cha shilingi milioni 482 kujenga stendi mpya ya kisasa ya mabasi katika kata ya Rundusi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa stendi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Mbunge wa jimbo la Songea Vijijini Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema kukalimika kwa mradi uo utaleta hamasa kubwa ya maendeleo kwa wananchi.
Mhagama amewaomba wataalamu na wasimamizi wa mradi kutanguliza uzalendo katika usimamizi pamoja na matumizi ya fedha kwani hatarajii kuona manunuzi wa vifaa vya mradi kuwa kichaka cha upotevu wa fedha.
“Tunaomba matumizi sahihi ya fedaha yajidhihilishe katika mradi huu hatutaki kuona ubabaishaji wa taarifa za manunuzi hivyo tusifanye makosa kwenye mradi huu wa stendi hatutapata mradi mwinge naomba tuendelee kufanya vizuri kama miradi mingine iliyopita” amesema Mhagama.
Hata hivyo Waziri Jenista amemshukuru Rais Dkt Samia Suhuhu Hassan kwa juhudi kubwa ambazo anazifanya katika kuleta Maendeleo kwa wananchi wake kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF
“Wananchi wezangu ni lazima tuwe na moyo washukrani kwa kuletewa miradi mingi ya TASAF hizi ni juhudi za Mheshimiwa Rais, hapa ninavyo zungumza milioni 482 zimeshaingizwa kwenye mfuko wa Halmashauri ili ujenzi wa stendi uanze mara moja” amesema Mhagama
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAASAF taifa Ndugu Shedrack Mziray amesema amefurahishwa na viongozi wa Halmashauri pamoja na Wananchi kwa usimamizi mzuri wa miradi ambayo imejengwa kwa fedha za TASAF kwani ni ishara ya uwajibikaji
Amesema lengo la serikali ni kuendelea kutoa ruzuku kwa walengwa pia na kutekeleza ujenzi wa miundo mbinu ya miradi ya kimkakati ambayo itasaidia kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya kupitia vikundu mbalimbali
“Miradi ya TASAF ni miradi shirikishi jamii kwahiyo jamii ndiyo iliyoibua na itasimamia usimamizi wote wa utekelezwaji wa miradi kupitia kamati ya usimamizi ya CMC nia yetu mradi huu ukamilike kwa viwango vinavyostahili” amesema Mziray
Amesema fedha zilizopokelewa kwa ajili ya mradi ni milioni 482 ambapo ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa vigae, ujenzi wa nguzo za umeme, eneo la kuegesha magari na ujenzi wa maduka 36 kuzunguka standi
Hata hivyo ameeleza mafanikio yatakayopatikana baada ya kukumilika kwa standi hiyo itarahisha usafiri kwa wananchi pamoja na kuongeza kipato kwa halmashauri kupitia wafanya biashara maeno ya standi pamoja na kuongeza ajira kwa vijana na wananchi wote kwa ujumla
“Kwa niaba ya wananchi wa halmshauri ya wilaya ya Songea tunapenda kumshukuru Rias wetu Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kazi nzuri anayoifanya ya kutuletea maendeleo katika nyanja zote na kutulea mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa wananchi wake” amesema magembe
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.