TARURA Mkoa wa Ruvuma imepokea shilingi milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika Wilaya ya Nyasa.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema fedha hizo zitafanya kazi ya ujenzi wa barabara ya Luhindo, Mpepo, Darpori kwa kiwango cha changarawe na madaraja.
“Lengo nikutaka kuwasaidia wananchi kwa kurahisisha usafiri na kuwatengenezea mazingira mazuri ya upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa kupitia mtandao wa barabara’’,alisisitiza.
Hata hivyo, amezitaja changamoto zinazoathiri utekelezaji wa mradi huo ni tabia ya wananchi kufanya ujenzi wa nyumba zao katika hifadhi ya barabara, kuchelewa kwa fedha za utekelezaji wa miradi hususani fedha za mfuko wa jimbo na mfuko wa barabara na wananchi kutupa takataka katika mifereji ya barabara husani.
Ameongeza kuwa TARURA inaendelea kutoa elimu kwa wananchi na kuzishirikisha Serikali za vijiji na mitaa katika kudhibiti zoezi la uendeshaji wa shughuli za kilimo pamoja na upitishaji wa mifugo barabarani.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.