SERIKALI imetoa zaidi ya shilingi milioni 800 kutekeleza miradi ya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Neema Maghembe amesema kati fedha hizo shilingi milioni 500 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili za upasuaji katika hospitali ya Halmashauri ya Songea iliyojengwa katika Kijiji cha Mpitimbi.
Kulingana na Mkurugenzi huyo fedha hizo katika hospitali hiyo zinajenga chumba cha kuhifadhia maiti,kichomea taka na nyumba moja ya mtumishi.
Maghembe amebainisha zaidi kuwa serikali pia imetoa zaidi ya shilingi milioni 200 kuboresha zahanati ya kijiji cha Mdunduwalo Kata ya Maposeni na kujenga nyumba ya familia mbili kwa ajili ya zahanati hiyo.
“Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan pia imetoa shilingi milioni 60 kwa ajili ya kujenga zahanati katika kijiji cha Matama Kata ya Muhukuru “,alisema.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo amepongeza Usimamizi unaofanywa kwenye miradi hiyo ambapo ameagiza ufuatiliaji wa karibu ili miradi yote ikamilike kwa wakati.
Hata hivyo ametahadharisha kuwa hujuma zozote kwenye miradi hazitavumiliwa ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha za miradi.Imeandikwa na Albano Midelo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.