SHAMBA LA MITI WINO LINAVYOCHOCHEA UCHUMI
Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wameanzisha shamba kubwa la miti lililopo Wino ambalo ni la tatu kwa ukubwa Tanzania .
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Kapenjama Ndile, amesema shamba hilo linaonesha jinsi ambavyo Songea haipo nyuma katika utunzaji wa mazingira, na shamba hilo linaweza kubadilisha na kuchochea uchumi wa nchi.
Amesema shamba hilo ambalo linasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS ) limekuwa likizalisha mbegu na miche mbalimbali na kusambaza kwa wananchi vijijini ili kuendelea kutunza mazingira na wawekezaji wakubwa wa kuchakata mazao ya misitu wako mbioni kujenga viwanda katika Halmashauri hiyo.
Kwa upande Meneja wa shamba hilo, Groly Kasmir, amesema shamba hilo lina ukubwa wa heka 39,714, kati ya hizo heka 2,259 zipo Wino, 29,000 zipo Ifinga na 9,000 zipo Mkongotema.
Ameeleza kuwa mpaka sasa miti waliyopanda ni misindano na mwaka huu wanatarajia kupanda miti aina ya mikaratusi kwa ajili ya nguzo kwa kuwa mazingira yanaonesha kuna uwezekano na miti hiyo kustawi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.