Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma kufanya msawazo wa walimu Kwa kupeleka walimu katika shule ya msingi lumaru Kata ya Upolo wilayani Nyasa, ikiwa imebakiwa na mwalimu mmoja baada ya walimu wanne kufariki Dunia Kwa Ajali ya gari iliyopinduka na kuwaka moto tarehe 28/12/2024 eneo la Burma wilaya ya Mbinga.
Ameyasema hayo wakati akiongoza mamia ya Wananchi wa wilaya ya Mbinga na Nyasa katika uwanja wa CCM Mbinga, kutoa heshima zao za Mwisho Kwa Ndugu jamaa na marafiki kwenye miili 6 kufuatia Ajali ya gari iliyopinduka na kuwaka moto.
Kanali Ahmed amefafanua kuwa wiki lijalo shule zinafungua hivyo amemtaka Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma kufanya Msawazo na kupeleka walimu katika shule ya msingi lumaru ili itakapofungua shule Wanafunzi wakute Kuna walimu.
Ameliagiza Jeshi la polisi kutoa elimu Kwa waendeshaji vyombo vya moto na Wananchi ili kuzuia Ajali za barabarani, badala ya kuwavizia na tochi na kuwatoza faini.
"Naliagiza Jeshi la polisi litoe elimu ya madhara ya mwendokasi na matumizi sahihi ya vyombo vya moto na Barabara badala ya kuvizia na tochi na kuwapigia faini madereva wanaoendesha mwendo Kasi, Kwa kuwa hii peke yake haitoshi"
Ametoa salamu za pole Kwa Wananchi ndugu jamaa na marafiki na kuwataka kushirikiana wakati wote wa shida na Raha.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Nyasa Bw.Khalid Khalif amewashukuru Viongozi wote na Wananchi Kwa ujumla Kwa kumfariji kipindi hiki kigumu na kumpa ushirikiano.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.