• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SIKU damu ilipogeuka mto,mashujaa 800 wa Litembo waliposimama kwa mishale dhidi ya bunduki 19

Imewekwa kuanzia tarehe: June 13th, 2025

Na Albano Midelo

 Jua lilipozama Machi 4, 1902, milima ya Umatengo haikulisindikiza kwa machweo ya kawaida.

Badala yake, anga lilitawaliwa na moshi mzito wa bunduki, vilio vya kina mama, na sauti za mwisho za mashujaa waliokataa kupigishwa magoti na mkoloni wa Kijerumani.

 Ni siku ambayo historia ya Tanzania ilichorwa kwa damu  na si damu ya kawaida, bali ya mashujaa wapatao 800, waliolala milele katika ardhi ya Litembo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kwa ajili ya kulinda heshima, ardhi, na uhuru wa kizazi cha leo.

Litembo: Jiwe Lililobeba Ujasiri

Katika kijiji kidogo cha Litembo,lipo jiwe kubwa linalofanana na kichwa cha tembo. Jiwe hilo si tu kivutio cha kijiografia, bali ni nembo ya ushujaa wa Wamatengo.

 Chini yake kuna pango refu lenye njia mbili moja ya kuingia, nyingine ya kutokea. Hapo ndipo mababu wa kabila la Wamatengo walijificha na kujipanga dhidi ya jeshi la wakoloni wa Kijerumani waliokuja wakibeba bunduki 19 na dhamira ya kutwaa ardhi kwa nguvu.

Mhifadhi na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mbinga, Mheshimiwa Ngwatura Ndunguru, anakumbuka historia hiyo kwa uchungu:

“Walituambia tushushe bendera yetu. Wakadai nchi hii sasa iko chini ya himaya ya Mjerumani. Wazee wetu walikataa. Hilo halikukubalika. Walijipanga, wakaingia mapangoni, wengine wakabaki nje kupambana. Wakoloni wakaanza kulimiminia risasi jiwe la Litembo. Watu wetu walipigwa risasi hadi kufa zaidi ya mia nane.”

Jiwe Lililotoa Damu, Mto Uliojaa Machungu

Picha ya maangamizi ilikuwa ya kusikitisha. Mto Litembo, uliokuwa chemchemi ya uhai kwa vijiji vya jirani, uligeuka kuwa mto wa damu.

Risasi za Wajerumani zilichuruzika kwenye ngozi za mashujaa wasio na silaha za kisasa. Walijibu kwa mishale, mikuki, na moyo wa ushujaa wa hali ya juu. Lakini hawakuweza kushindana na risasi za moto.

Katika machafuko hayo, mashujaa waliouawa walizikwa kwenye makaburi ya pamoja, yaliyopewa jina la Hola Hola. Salvius Simon Komba, Mwenyekiti wa Mila kata ya Litembo, anasimulia:

“Lile pango lilitumika kuhifadhi miili. Linaweza kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja. Lakini idadi ya waliokufa ilizidi uwezo wake. Hata leo, ukichimba ardhini eneo hili, utakuta masalia ya miili  mifupa, vichwa, hadi mabaki ya silaha za jadi.”

Ukatili wa wakoloni haukuishia kwenye bunduki

Ukatili wa wakoloni haukuishia tu kwa risasi. Waliamua kuchoma maghala ya chakula, kuteketeza nyumba, na kuacha jamii nzima ya Wamatengo ikikumbwa na njaa kali.

Bruno Tembo, Katibu wa Baraza la Mila kata ya Litembo, anakumbusha kuwa, kiongozi wa Wajerumani aliyejulikana kama Korongo, ndiye aliyetoa amri ya shambulio hilo baada ya Chifu Kawania wa Wamatengo kukataa kushirikiana naye.

“Baada ya mashujaa wetu kukataa kutawaliwa, Korongo alileta askari na silaha. Lakini mababu zetu walijipanga. Walijificha kwenye pango, wengine walikaa nyuma ya jiwe. Vita ikaanza. Lakini walizidiwa na risasi.”

Mnara wa Kumbukumbu: Alama ya Mashujaa Waliosahaulika

Mnamo mwaka 2004,Mbunge Mstaafu Mheshimiwa  Ngwatura Ndunguru alisimamia ujenzi wa mnara wa kumbukumbu katika eneo la jiwe la Litembo.

Mnara huo, uliowekwa maandishi ya sonara, ni alama ya heshima kwa waliolala milele kwa ajili ya kizazi hiki.

“Maandishi yameanza kufifia, lakini ujumbe wake bado unaishi. Mnara huu unahitaji ukarabati na eneo hili lina kila sifa kuwa Makumbusho ya Kitaifa, lakini bado halijatambuliwa rasmi. Ni wakati sasa Serikali ichukue hatua,” anasisitiza Ndunguru.

Litembo si tu historia ya Mbinga. Ni historia ya Taifa. Ni mfano hai wa mapambano ya kiafrika dhidi ya ukoloni. Ni eneo linalopaswa kuwa darasa la historia, kivutio cha utalii wa kihistoria, na kitovu cha uzalendo wa kizazi kipya.

Salvius Nyamajabeni, Mwenyekiti wa Baraza la Mila tangu 1958, anatoa rai nzito:

“Hatuwezi kuendelea kuwasahau mashujaa waliotufia. Serikali iwekeze hapa. Tuoneshe kizazi kipya kwamba uhuru hauna thamani kama hatukumbuki damu iliyomwagika kuupata.”

Litembo ni zaidi ya jiwe. Ni kaburi la mashujaa 800, darasa la kizazi, na ukumbusho wa bei ya uhuru. Tunapokimbizana na maendeleo ya kisasa, tusisahau walikodondoka mashujaa wetu.

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAKULIMA Ruvuma waomba soko la mahindi kufunguliwa haraka

    June 16, 2025
  • SERIKALI ,dini na wananchi Ruvuma waungana kudumisha amani

    June 16, 2025
  • RUVUMA yaandika historia chupa 4040 za damu zakusanywa kuokoa maisha

    June 15, 2025
  • NAMTUMBO yaagizwa kuongeza kasi ya kushughulikia hoja za CAG

    June 15, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.