TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imeokoa fedha za umma zaidi ya shilingi milioni 107 kutokana na uchunguzi mbalimbali unaoendelea kufanywa.
Akitoa taarifa hiyo katika ukumbi wa TAKUKURU Songea Mjini Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amesema Fedha iliyookolewa ni kutoka benki ya wananchi Mbinga(MCB) zaidi ya shilingi 488.
Fedha nyingine iliyookolewa ni kutoka zaidi ya shilingi milioni 94 toka chama vya kuweka na kukopa( SACCOS ) Wilaya ya Songea na Marejesho ya madeni ya Muungano (SACCOS) wilayani Namtumbo zimeokolewa sh.1,779,000 na marejesho ya madeni Mbinga Teachers SACCOS sh.2,465,000 na kwamba fedha za SACCOS zimewekwa kwenye akaunti ya vyao vyao.
“shilingi5,890,000 ni fedha iliyookolewa wilayani Nyasa kwenye deni feki alilowekewa ndugu Ufunuo Chirwa na mtu wa Taasisi ya Maboto,alistahili kulipwa shilingi 4,000,000 lakini aliwekewa deni la jumla ya sh9,890,000 kwa njia ya ujanja’’,alisema Mwenda.
Amesema katika kipindi hicho TAKUKURU ilifuatilia miradi ya maendeleo nane yenye thamani ya shilingi bilioni 3.345 na kuitaja miradi iliyokuwa inafuatiliwa na TAKUKURU ni Elimu,Barabara na Maji.
Amesema wamejipanga kuelimisha wananchi kupiga vita rushwa dhidi ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Imeandaliwa Aneth Ndonde na Farida Mussa
Kutoka ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Octoba 24, 2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.