MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa rai kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Mkoa wa Ruvuma kuhudhuria katika tamasha la utalii wa fukwe Mkoa wa Ruvuma linalotarajia kufanyika kuanzia Desemba 19 hadi 20 mjini Mbambabay wilayani Nyasa.
Mndeme amesema Mkoa wa Ruvuma hufanya tamasha la utalii wa fukwe kila mwaka lengo likiwa kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Nyasa vikiwemo fukwe za asili za ziwa Nyasa,samaki wa mapambo na simba weupe waliopo katika Pori la Akiba la Liparamba.
Vivutio vingine amevitaja kuwa ni mawe makubwa yaliyopo ndani ya ziwa Nyasa likiwemo jiwe la Pomonda,visiwa vizuri vya kuvutia ndani ya ziwa Nyasa vikiwemo kisiwa cha Lundo,Zambia na Puulu pamoja na ngoma za asili zilizopo mwambao mwa ziwa Nyasa ambazo zina utangaza Mkoa wa Ruvuma.
“Karibuni wageni wote kutoka ndani ya Mkoa na mikoa jirani ,katika tamasha la safari hii kutafanyika michezo ya ufukweni na ngoma za asili ili kutangaza utamaduni katika Mkoa wetu’’,alisema.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.