Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma imeidhinishiwa kutumia shilingi 1,116,513,478.28 kutoka bodi ya mfumo wa barabara Kwa ajili ya matengenezo ya barabara na utawala.
Akitoa taarifa kwenye kikao Cha kamati ya ushauri wilaya (DCC) kwa niaba ya Meneja wa TARURA Mhandisi Albert Mtimba alisema zaidi ya BILIONI 1.1 zimeidhinishwa kutumika katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Mtimba amesema kiasi hicho Cha fedha kitatumika kuhudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya kilomita 975.254 na madaraja 74.
Aidha Mtimba alifafanua kuwa katika kilomita 975.254 kilomita 4.603 ni barabara za Lami sawa na asilimia 0.47. na kilomita 280.369 barabara za changarawe sawa na asilimia 28.75.
Mtimba alisema kilomita 690.281 ni barabara za udongo ambapo ni sawa na asilimia 70.79za barabara za wilaya ya Namtumbo.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo akiwemo Diwani wa kata ya Litola Mheshimiwa Paulo Kamilius Fussi walizungumzia kitendo Cha utengenezaji wa barabara wakati wa masika na kusababisha usumbufu Kwa watumiaji wa barabara hizo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.