Jumla ya Kaya 67,780 na vijiji 685 vinanufaika na Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Mkoa wa Ruvuma.
Hayo amesema Mratibu wa TASAF Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira ofisini kwake kuwa Mpango huo wa awamu ya tatu kipindi cha pili 2020-2023 unatekelezwa katika Halmashauri zote nane.
Amesema utekelezaji wa kipindi hiki unatekelezwa katika Vijiji,Mitaa yote ambayo haikufikiwa katika utekelezaji wa kipindi cha kwanza ikiwa na lengo kuu la kuwezesha Kaya maskini kuongeza kipato pamoja na fursa.
Mlimira amesema Mpango wa TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili unasehemu kuu nne za utekelezaji kwa kutoa ruzuku kwa Kaya Maskini hususani kaya zenye watoto ili ziweze kupata lishe bora pamoja na huduma za Elimu na Afya.
Kutoa ajira za muda kwa Kaya maskini zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi,kuongeza kipato kwa Kaya kupitia Vikundi vya Uwekezaji,kuwekeza kwenye shughili za uchumi ili kuboresha maisha.
Mratibu amesema malengo hayo ni pamoja na kujenga uwezo katika ngazi zote za utekelezaji kupitia mafunzo na utekelezaji pamoja na kuboresha miundombinu ya sekta ya Elimu Maji na Afya.
Hata hivyo Mratibu amesema msisitizo wa kipindi cha pili utalenga kuwezesha Kaya maskini kufanya Kazi na kuwezesha kipato na kuongeza rasilimali zalishi pamoja na kuongeza vitega uchumi.
Kuwekeza kwa Watoto ilikuleta matokeo chanya yatakayodumu kwa mda mrefu,kuboresha huduma za upatikanaji wa Maji,Afya na Elimu pamoja na kukuza uchumi wa eneo linalofanyika utekelezaji kutokana na matokeo ya mpango.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 6,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.