Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ruvuma imepiga hatua kubwa katika kuongeza idadi ya wafanyabiashara wanaojiandikisha kulipa kodi .
TRA imendelea kuongeza makusanyo ya mapato, kufuatia jitihada za makusudi kuboresha mahusiano na walipakodi kupitia programu za elimu ya kodi.
Kwa kutumia mikutano ya kijamii, semina, na vikao vya ushauri wa kodi, TRA imeweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwaelimisha kuhusu wajibu wao wa kulipa kodi.
, Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Walipakodi wa TRA Ruvuma, Hilary Gerald, amesema kampeni ya kutoa elimu imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mwitikio wa hiari kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara katika kulipa kodi.
Amesema hali hiyo I mechangia kwa kiasi kikubwa kubadilika kwa mtazamo wa wananchi kuhusu ulipaji kodi na kuimarisha mapato ya Serikali.
Gerald ametoa rai kwa walipakodi wote kuhakikisha wanalipa awamu ya pili ya kodi kabla ya tarehe 31 Mei 2025, huku akisisitiza kuwa mwisho rasmi wa malipo hayo ni tarehe 30 Juni 2025.
Wafanyabiashara wamekumbushwa kutoa risiti za kielektroniki (EFD) kwa kila mauzo, huku wanunuzi wakihimizwa kudai risiti hizo ili kusaidia kuimarisha mfumo wa mapato ya taifa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.