HALMASHAURI ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imetoa mkopo wa shilingi milioni 240 ambayo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha vijana,wanawake na wenye ulemavu .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Gasper Balyomi amekutana na kufanya mazungumzo na Wanufaika wa mkopo wa Halmashauri hiyo ambapo wanufaika hao ni Wanawake asilimia nne, Vijana asilimia nne na Walemavu asilimia mbili.
Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Tunduuru imetenga kiasi cha shilingi 240 kwajili ya kuwakopesha Wanawake, Vijana na Wenye ulemavu ambayo ni asilimia kumi inayo takiwa kutolewa kwa vikundi hivyo kwa kipindi cha mwaka wa fedha .
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amevipongeza vikundi vya Wanawake kwa kuonesha mwenendo mzuri wa kurejesha mkopo huo ambapo ametoa rai wananchi wajiunge katika vikundi ili wanufaike na mkopo huo wa Halmashauri na kusisitiza vikundi ambavyo wamekopa mkopo na hawajaresha mikopo yao warejeshe mikopo kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kukopa.
“kwa vikundi ambavyo vinakopa na kurejesha mikopo yao kwa wakati vitapewa kipaumbele na kuongezewa kiwango cha mkopo”,alisema na kuongeza kuwa hadi sasa kuna vikundi vinarejesha vizuri marejesho.
Imeandikwa na Afisa Habari Halmashauri ya Tundurui
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.