Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahamed Abbas Ahamed, amesema kuwa Mkoa wa Ruvuma hali ya maambukizi imepungua kutoka asilimia 5.6 mwaka 2016/2017hadi kufikia asilimia 4.9 mwaka 2023 sawa na asilimia 0.7ya kiwango kilichopunguwa ambapo halmashauri ya manispaa ya Songea inaongoza ikifuatiwa na halmashauri ya Tunduru.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo leo wakati akizindua Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani katika viwanja vya Michezo vya majimaji, ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Ruvuma katika Manispaa ya Songea mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philipo Mpango.
Kuhusu hali ya UKIMWI mkoani Ruvuma takwimu zinaeleza kuwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi (VVU) wapo 68,237 ambao wanaume ni 24,959 sawa na asilimia 37 ,Wanawake 43,000 sawa na asilimia 63 ,watoto chini ya umri wa miaka 15 wapo 2,382 sawa na asilimia 3.5 na watu wazima kuanzia umri wa miaka 15 wapo 65,855 sawa na asilimia 96.5.
" Ndugu viongozi pamoja na wananchi halmashauri zetu zinazoongoza ni maspaa ya Songea ikifuatiwa na Tunduru lakini vile vile na halmashauri ya Mbinga hivyo napenda kuchukuwa fursa hii kutoa wito kwa wananchi wote kuzingatia tiba na matunzo lakini vile vile kuendelea kutumia dawa za kufubaza kwani hiyo njia pekee ya kuendelea kupambana na matatizo haya" alisema Kanali Ahamed Abbas Ahamed.
Alisema kuwa siku hii ya ufunguzi ni muhimu kwa kuelimisha umma kuhusu janga la UKIMWI, kuhamasisha kupunguza maambukizi mapya, na kuongeza juhudi za matibabu na huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (VVU).
Katika uzinduzi huo, Kanali Ahamed alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii, serikali, na wadau mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huu. Hii ni sehemu ya jitihada za kitaifa kuendeleza elimu na ufahamu kuhusu UKIMWI, na kudumisha haki za watu wanaoishi na virusi hivyo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Afya Dkt. Catherine Joachim Mkuu wa Program ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na wananchi wake kwa kupiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwa ushamiri wa VVU umeshuka kutoka asilimia 5.6 mwaka 2016/17 mpaka asilimia 4.9 mwaka 2022 .
Alisema kuwa takwimu hizo zinaonesha Mkoa wa Ruvuma unaongoza katika upimaji wa VVU hata hivyo Mkoa umeendelea kufanya vizuri katika VVU vya 95/95/95 ambapo ushamiri wa utafiti wa mwaka 2023 tumeonesha asilimia 82 ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanatambua hali zao za maambukizi na asilimia 97 ya walioambukizwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi na asilimia 99 ya wanaotumia dawa za kufubaza tayari wameshafubaza virusi jambo ambalo linaoneaha Mkoa huo umepiga hatua kubwa sana ikili ganishwa na mwaka 2016/17.
" Japokuwa Mkoa upo nyuma ukilinganisha na wastani wa Kitaifa wa 95/95/95 ambapo 95 ya kwanza Kitaifa tupo asilimia 83, 95 ya pili tupo asilimia 98 na 95 ya Tau tupo asilimia 94" alisema Dkt. Catherine Joachm.
Alieleza zaidi kuwa kutokana na Mkoa wa Ruvuma umeendelea kukuwa kiuchumi kupitia shughuli za kilimo ,migodi ya makaa ya mawe na madini mengine, usafirishaji na uvuvi maendeleo hayo yamepeleta nakisi kubwa kwenye usawa unaopelekea baadhi ya makundi kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi ya VVU.
Aidha alisema kuwa uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa Vijana wa kike kati ya miaka 15 na 24 wameendelea kuwa katika hatari hasa katika miji na vitongoji yanakopita maroli yakusafirisha makaa ya mawe kwenye machimbo madogo madogo na kwenye shughuli za uvuvi.
Naye Mwakilishi wa Baraza la watu wanaoishi na VVU na mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la NACOPHA Letisia Moris alisema kuwa hali ya unyanyapaa na ubaguzi wa VVU bado ni changamoto ndani ya Jamii hivyo uhathiri juhudi za kutokomeza Ukimwi wakati ni sawa kwa Kila Mmoja kuzingatia kauli mbinu ya mwaka huu inayoimiza juu ya mabadiliko ya tabia inayosema chagua njia sahihi ,tokomeza UKIMWI.
" Niwaombe viongozi wa dini, viongozi wa kimila na serikali kwa nafasi zao kuwa msatri wa mbele katika kukemea vitendo vya udhalilishaji ,unyanyapaa na ukatili kwa watu wanaoishi na VVU kwa kufanya hivi tutakuwa na Jamii iliyostaraabika na yenye uwelewa mkubwa wa namna ya kuheshimu haki za binadamu." Alisema Letisia
Hata hivyo ametia wito kwa wanaotunga Sera na mikakati ya kupambana na VVU kuzingatia vipaumbele vya Jamii hususani kwa Vijana katika utekwlezaji wa mipango ili kuharakisha upatikanaji wa matokeo chanya ifikapo mwaka 2030.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.