MWENYEKITI wa Jumuiya ya wafanyabiashara Taifa Khamis Livembe Abdallah ameongoza Mkutano wa wadau wa Biashara Mkoa wa Ruvuma na kujadili changamoto mbalimbali.
Akizungumza katika Mkutano huo uliojumuisha wadau kutoka mikoa ya Njombe,Iringi pamoja na Ruvuma katika ukumbi wa Familia takatifu Bombambili Manispaa ya Songea amesema Mkoa wa Ruvuma Changamoto zimeshughulikiwa ukitofautisha na Mikoa Mingine.
“Niipongeze Serikari ya Mkoa kwa kutatua changamoto za wafanyabiashara na mengi yametatuliwa,ikiwemo TRA ya Mkoa wa Ruvuma ni Mfano ya Mikoa Mingine “.
Abdallah amesema hoja nyingi ambazo wafanyabiashara wamezitaja ni za kisera ambazo kama mamlaka hawahusiki ikiwemo kodi ya zuio.
Naibu Katibu Mkuu wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt.Hashil t.Abdallah katika mkutano huo amempongeza Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Taifa kwa kazi kubwa ya kuiongoza Jumuiya hiyo na uongozi thabiti na mahusiano katika Serikali yameimalika.
Abdallah amesema Wizara na Serikali kwa ujumla lazima waweke mazingira wezeshi ili mfanyabiashara afurahie kazi yake na Serikali imlee na kumwezesha Mfanyabiashara na Serikali iweze kukusanya kodi na watu wajipatie ajira.
“Tumeshudia mara kadhaa migongano katika Jumuiya Mbalimbali lakini Jumuiya ya Wafanyabiashara imekuwa ya Mfano inawaunganisha na kuwa na sauti moja juu ya yale yanayowatatiza”.
Abdallah amesema wafanyabiashara maamuzi ya kukaa pamoja na kutafakari kwa pamoja baina ya wafanyabiashara na viongozi wa Mkoa ni jambo jema ambalo linapelekea kuleta maendeleo katika Taifa la Tanzania.
“Tupo hapa kumwakilisha Mama Yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia ametuagiza tusiondoke na kero lazima tumalize hapa hapa “.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Juni 28,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.