SERIKALI kupitia Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,imetenga zaidi ya Sh.milioni 80 kwa ajili ya kuchimba visima vinne vya maji ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa mji wa Tunduru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Chiza Marando ameyataja ,miongoni mwa maeneo ya kuchimba visima ni soko kuu la Azimio,soko la Nanjoka,kituo kikuu cha mabasi na maeneo mingine yanayotumika kupakia na kushushua watu wanaotoka pembezoni mwa mji wa Tunduru.
Marando amesema ,wameamua kuchimba visima hivyo katika maeneo tofauti yenye uhitaji wa maji na kwamba maji hayo yataingizwa kwenye mfumo wa mabomba kabla ya kusambazwa wananchi .
“Halmashauri tumeamua kushirikiana na Mamlaka ya Maji mjini Tundur (TUUWASA ) ili kuhakikisha wanapunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika mji wa Tunduru”,alisema.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema ,maji hayo yatauzwa na kuwa sehemu ya chanzo cha mapato ya Halmashauri.
Marando,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa magari ya kuchimba visima vya maji kwa kila mkoa hapa nchini na amewaomba wananchi kushirikiana na serikali yao katika ulinzi wa visima na miundombinu ya maji itakakayojengwa katika maeneo mbalimbali.
Msimamizi wa uchimbaji visima kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Kanda ya Kusini Thomas Masheyo amesema ,utafiti unaonesha kuwa eneo kubwa la mji wa Tunduru lina maji mengi ambayo yanatosheleza mahitaji ya watu wa mji huo.
Ameshauri wananchi wanaotaka kuchimba visima ni vyema kuzingatia ushauri wa wataalam kwa kuchimba visima virefu badala ya vifupi kwa kuwa maji ya juu yanayopatikana kwenye visima vifupi siyo salama kwa matumizi ya binadamu.
Mfanyabiashara wa Soko la Azimio mjini Tunduru Andrew John amesema ,maji hayo yatamaliza adha kubwa ya maji katika soko hilo ambalo kwa muda mrefu halina maji ya uhakika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.