Upungufu wa mbolea mkoani Ruvuma na nchi nzima kwa ujumla utabaki historia baada ya kiwanda cha mbolea cha ITRACOM kuzalisha mbolea inayokidhi mahitaji ya mbolea ya wakulima kwa mwaka.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Kiwanda cha ITRACOM FERTILIZER LIMITED Dkt Keneth Masuki wakati anazungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa ghala la mbolea la kiwanda hicho mtaa wa Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Dkt Masuki amesema kiwanda hicho cha mbolea ambacho kimejengwa mkoani Dodoma kina uwezo wa kuzalisha mbolea na virekebishi vya udongo zaidi ya tani milioni 1.5 kwa mwaka hivyo kukidhi mahitaji ya mbolea katika nchi nzima ambayo ni kati ya tani 600,000 hadi 700,000 kwa mwaka.
“Uwekezaji wa kiwanda hiki ni wa kimkakati kwa sababu Mheshimiwa Rais alipokuwa Makamu wa Rais ndiye aliyeanza hizi harakati za uwekezaji wa kiwanda,mchakato ulianza mwaka 2020,uwekezaji ni mkubwa kwa kuwa kiwanda ni kikubwa ambacho kinailetea heshima Tanzania’’,alisisitiza Masuki.
Ameongeza kuwa katika Bara la Afrika hakuna kiwanda kikubwa cha mbolea kama hicho ambacho kinatengeneza mbolea iliyochanganywa mbolea za chumvi chumvi na samadi ambapo amesema kiwanda kimetokana na Mwekezaji ambaye alikuwa na kiwanda kama hicho nchini Burundi.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa ghala la kiwanda cha ITRAFOM,mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mheshimiwa Kapenjama Ndile amesema matokeo ya kiwanda hicho ni jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye alifanya juhudi za kumshawishi Mwekezaji ili kuhakikisha kiwanda cha mbolea kinaanzishwa nchini kukidhi mahitaji ya wakulima.
Amesisitiza kuwa kufunguliwa kwa ghala hilo mjini Songea ni fursa ya kiwanda hicho kifungua maghala mengine mengi ya mbolea maeneo ya vijijini waliko wakulima wengi.
“Nimeambiwa ITRAFOM inatengeneza aina tatu za mbolea ambazo ni mbolea ya kupandia(FOMI PANDIA),mbolea za kukuzia (FOMI KUZIA) na mbolea za kuzalisha (FOMI NENEPESHA) ni matumaini yangu kuwa wakulima watajengewa uwezo kuhusu namna ya kutumia mbolea hii ili uzalishaji uwe na tija’’,alisisitiza.
Amebainisha kuwa katika msimu wa mwaka 2022/2023 wakulima mkoani Ruvuma wamezalisha tani 1,870,800 ya mazao ya chakula,biashara na mbogamboga na saw ana asilimia 95 ya lengo la mavuno ya tani 1.965,072 .
Hata hivyo amebainisha kuwa kwa mazao ya chakula pekee katika kipindi hicho zilivunwa tani 1,598,163 na mazao ya biashara zilivunwa jumla ya tani 94,741.
Amesisitiza kuwa uzalishaji mkubwa wa mazao katika mkoa wa Ruvuma ulitokana na matumizi makubwa ya mbolea ambapo katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa ulitumia zaidi ya tani 71,000 na kwamba katika msimu huu wa mwaka 2023/2024 hadi sasa tani zaidi ya 41,000 za mbolea zimesambazwa kwa wakulima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.