Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Mwl. Edith Mpinzile amewahimiza walimu kutenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya na utimamu wa akili kwa lengo la kuepuka msongo wa mawazo katika kutekeleza majukumu ya ufundishaji.
Mpinzile ametoa wito huo wakati anafunga bonanza la michezo kwa walimu wa Sekondari na Msingi ambalo liliwakutanisha walimu kutoka Halmshauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma,ambalo limefanyika katika uwanja wa Chandamali mjini songea
Mpinzile amesema kushiriki michezo si kuimarisha afya pekee bali pia inasaidia kujenga mahusiano sehemu za katika kazi na kupata muda wa kujadili mambo mbalimbali ya kitaaluma
“Nipende kuwapongeza kwa kushiriki katika bonanza hili kwani sote tunafahamu kuwa michezo ni afya lakini mbali ya kufahamu hivyo niseme tu kuwa michezo inatuunganisha na kutuweka pamoja” alisema Mpinzile.
Katika ufungaji wa bonanza hilo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ambaye aliwakilishwa na Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.