Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Ndugu. Jumanne Mwankhoo amewataka wadau wa kilimo kutoa Elimu sahihi ya matumizi ya pembejeo za kilimo kwa wakulima ili waweze kupata matokeo mazuri.
Amesema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa kilimo kuelekea msimu mpya wa kilimo wa mwaka 2024/25 kilichowajumuisha maafisa kilimo na wauzaji wa pembejeo za kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa Heritage Cottage mjini Songea.
"Niwasihi wadau wote wa kilimo tuendelee kushirikiana ili kuhakikisha elimu sahihi inafika kwa wakulima, niwaombe wauzaji wa pembejeo tuwashauri wakulima ipasavyo, tusiwashauri tu kwa maana ya tunataka tuuze,"alisema Ndg. Mwankoo.
Nae Afisa kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Onesmo Ngao, amesema tayari wametoa vibali kwa Makampuni na wadau wa kilimo kutoa Elimu kwa wakulima katika Halmashauri.
Ameongeza kuwa suala la Elimu ni mtambuka hivyo wadau wote wanatakiwa kwenda kwenye maeneo ya kazi na kuwafikia wakulima ili kutoa Elimu.
Kwa upande wake Mkaguzi wa Mbegu kutoka Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Kapaya Said, ameeleza namna ambavyo Serikali imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanauza mbegu boraa na sahihi.
Ameongeza kuwa mbegu zote za mahindi za msimu wa kilimo wa 2024/25 zinatakiwa ziwekwe katika mfumo wa kidijitali na kuuzwa kwa mfumo wa ruzuku ambapo tayari Makampuni ya uuzaji wa pembejeo yanaendelea kuweka mbegu katika mfumo huo.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwa shughuli za kilimo hususani uzalishaji wa zao la mahindi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.