Wakulima wa kahawa wanaohudumiwa na Chama cha Msingi cha Ushirika Kimuli Amcos, kata ya Utiri, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, wamefanikiwa kuzalisha tani 105,986.95 za kahawa na kupata mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 14 kuanzia msimu wa 2021/2022 hadi 2024/2025.
Katibu wa chama hicho, Aron Komba, amesema uzalishaji huo umeendelea kuimarika kila msimu, huku wakulima wakifaidika na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya kahawa.
Kwa mujibu wa Komba, katika msimu wa 2021/2022 wakulima walizalisha tani 548,551 zenye thamani ya shilingi bilioni 3.3, huku msimu wa 2022/2023 wakizalisha tani 455,643 na kupata shilingi bilioni 3.06. Msimu wa 2023/2024 ulirekodi uzalishaji wa kilo 585,288 za kahawa zenye thamani ya shilingi bilioni 2.9, na kwa msimu wa 2024/2025 uzalishaji ulifikia kilo 530,253, huku kahawa hiyo ikiuzwa kwa shilingi bilioni 4.72 kupitia minada.
Hata hivyo amesema mafanikio haya yametokana na jitihada za Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mikopo ya pembejeo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.05 kwa wakulima 7,005 wa kahawa na mazao mengine. Msimu wa 2022/2023, wakulima 2,137 walipata mikopo ya shilingi milioni 957, huku msimu wa 2023/2024 wakulima 2,381 wakipata shilingi milioni 917. Msimu wa 2024/2025, mikopo iliongezeka hadi shilingi bilioni 1.18 kwa wakulima hatua iliyosaidia kuboresha uzalishaji.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Utiri, Libaba Gervas Libaba, ameiomba Serikali kupitia TARURA kukamilisha ujenzi wa barabara ya lami ya Utiri-Mahende ili kurahisisha usafirishaji wa kahawa kutoka mashambani hadi sokoni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.