Pichani ni mkazi wa kijiji cha Mtonya Issa Yasin akitoa salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kununua korosho za wakulima kwa bei nzuri ya shilingi 3,300 kwa kilo.
Salamu hizo amezitoka mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wakati alipofanya ziara ya kukagua mwenendo wa uuzaji wa korosho katika kijiji cha Mtonya wilaya ya Tunduru jana (Jumatano 21,Novemba 2018)
Mkulima Yasin amefanikiwa kuuza tani 4 na kilo 200 za korosho na kujipatia kiasi cha shilingi milioni 13.8 katika msimu wa 2018/2019 kwa bei ya 3300.
Akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara Mkuu wa Mkoa Mndeme amewahakikishia wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma ambao wanalima zao la korosho kuwa serikali ya awamu ya Tano itanunua korosho zote kwa elekezi na kuwa fedha kwa kazi hiyo zipo.
"Napenda kupokea salamu za pongezi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli kama mlivyosema,nitafikisha kwake salamu hizi" alisema Mndeme kwenye mkutano wa wananchi wa kijiji cha Mtonya
Aidha ,amewaonya wafanyabiashara ambao watajihusisha na biashara haramu za Kangomba kuwa vyombo vya dola vipo makini kuhakikisha kuwa wanadhibiti biashara hiyo ili kumwezesha mkulima kupata bei nzuri ya korosho zake.
Kwa mujibu wa takwimu za mkoa wa Ruvuma hadi kufikia tarehe 11 Novemba 2018 jumla ya kilo 2,690,261 sawa na tani 2,690 za korosho zilikuwa zimepokelewa kwenye maghala makuu katika wilaya ya Tunduru.
Mwisho
Zao la korosho katika mkoa wa Ruvuma linalimwa kwenye wilaya za Tunduru,Nyasa,Songea na Namtumbo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.