SERIKALI imetoa shilingi milioni 67 kutekeleza mradi wa Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Mahande Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji Mkoani Ruvuma.
Wakati akisoma taarifa mbele ya kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Ruvuma, Mtendaji wa Kata ya Utiri Barclay Mwarabu amesema mradi huo umegharimu kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 67 .
Mwarabu ameeleza fedha hizo zimetumika kununulia vifaa vya ujenzi viwandani na kulipa mafundi kwa shughuli mbalimbali za ukamilishaji wa mradi.
“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kutujengea zahanati hii maana ametutatulia changamoto kubwa ya huduma ya afya katika kijiji chetu”, amesema Mwarabu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.