Na Gustaph Swai-RS Ruvuma
Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amewataka Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha Mbwa wote wanachanjwa na kufungiwa ndani mda wote wa Mchana.
Ametoa wito huo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa duniani yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya kata ya Matarawe wilayani Songea.
"Serikali inaposisitiza kuhakikisha Mbwa wote wanachanjwa na wanafungiwa ndani mda wote wa Mchana inakusudia kuhakikisha kuwa watu wanafanya shughuli zao za maendeleo bila kikwazo cha woga wa kupata kichaa cha Mbwa au kujeruhiwa na Mbwa", alisema.
Kapenjama amewaasa wananchi kushirikiana kuhakikisha wanatoa taarifa kwa Ofisi husika wanapoona Mbwa wanazurura mchana au wanapokuwa na taarifa ya Mbwa wasio na wamiliki.
Ametoa rai kwa Wananchi kutafakari namna wanavyoshiriki katika kuthibiti ufugaji holela wa Mbwa kwani katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawataka kuwapa Mbwa huduma zote za Msingi kama Chakula, Matibabu na malazi.
Sanjari na hayo amewataka wale wanaotumia Mbwa katika shughuli za kuchunga mifugo au kuwinda kuwaweka chini ya uangalizi Mbwa wao ili wasidhuru watu wengine.
Naye Daktari wa Mifugo Manispaa ya Songea Seria Shonyela amebainisha kuwa Manispaa ya Songea ina Mbwa zaidi ya Elfu10 na kuwasihi wananchi kujitokeza kuchanja Mbwa wao na kupunguza Mbwa wasio na wamiliki.
Kwa upande wake Mwananchi anayemilikii Mbwa Hendrick Mbena ameishukuru Serikali kwa kutoa chanjo ya kichaa cha Mbwa bure na kuwahimiza Wananchi wengine kujitokeza kuchanja Mbwa wao ili kuunga juhudi za Serikali za kuzuia madhara ya kichaa cha Mbwa.
Kichaa cha Mbwa ni Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Kichaa cha Mbwa na huathiri wanyama wote hususani Mbwa na binadamu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.