Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kujijengea tabia ya kulipa kodi ya pango ya Ardhi kwa wakati kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuondokana na riba kila mwaka
Hayo yamezungumzwa na Mtathini na Mratibu wa kodi ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma, Herbert Mwaleka, wakati alipokuwa akitoa Elimu kwa Wananchi wa Kata ya Ruhuwiko Songea, kwenye hafla ya kuwakabidhi hati za viwanja Wananchi hao
Alisema kwa wale wote watakao kabidhiwa hati za Ardhi watambue kuwa wao ni wapangaji katika Aridhi hizo hivyo niwajibu wao kila mwaka kuzilipia Ardhi zao, kwani kwakufanya hivyo wataepukana na riba pia amewasisitiza kujijengea tabia ya ulipaji pango ya Ardhi
“Kila mwenye kipande cha Aridhi lazima atambue wajibu wake katika kumiliki kiwanja hicho kwa sababu niwajibu wake kila mwaka kulipa kodi ya pango ya Ardhi kwa maana usipo ilipa kwa wakati kunakuwa na riba niwasihi Wananchi wa Ruhuwiko kanisani usipo lipa kwa wakati ikaongezeka riba ya asilimi 0.5 hivyo tutimize wajibu wetu”, ailisema Mwaleka,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.