MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr,Jairy Nkhanga ametoa rai kwa wananchi kushirikishwa katika mapambano dhidi ya virusi hatari vya corona.
Dr. Nkanga ametoa rai hiyo kwenye kikao cha Kamati ya Maafa ya Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Songea kilicho fanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya songea.
Amesema ni vema katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona wananchi wakashirikishwa hasa wa maeneo ya vijijini kwa kutoa taarifa kuhusu wageni wanaoingia mkoani Ruvuma ambao hawawatambua na kutoa taarifa za wageni hao kwenye Mamlaka ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa na vyombo vinavyohusika sambamba ufuatiliaji wa karibu kuhusu washukiwa.
“Changamoto za miundombinu na vitakasa mikono na barakoa zisirudishe nyuma mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona badala yake taratibu na miongozo ya serikali kupitia Wizara ya Afya’’,alisema.
Aidha amewashauri Waganga Wakuu wa Wilaya zote kuchukua hatua za makusudi kununua vitakasa mikono na barakoa kwenye muduka ambako vifaa hivyo vinapatikana badala ya kusuburi kuagiza Bohari kuu ya madawa ya Serikali kufuatia unyeti wa suala la mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona
Mkuu wa wilaya ya songea pololeti mgema ametaka magari yote wanayobeba wageni ya puliziwe dawa ya kuua wadudu wakiwemo wa corona
Imeandaliwa na Ofisi ya Habari Manispaa ya Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.