Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Menace Komba, amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuwahamasisha wananchi kulima mazao ya biashara.
Hayo ameyasema kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, walipokuwa wakipitia taarifa mbalimbali za miradi ya halmashauri hiyo.
Alisema serikali ipo kwa ajili ya kumilinda mkulima, pia imeweka mfumo mzuri wa kuyauza mazao hayo hivyo madiwani wezangu tuzidi kuwahimiza wananchi katika kilimo cha biashara kwani kinatija vile vile soko bado linahitaji mazao hayo.
“Kuna vikwazo wakulima wetu wanakutana navyo asa kwenye kipindi cha kuuza mazao yao, halmashauri yetu haijawai kukutana na changamoto yoyote kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani ila changamoto ni watanzania wezetu ambao wana warudisha nyuma wakulima ila tunawashugulikia ili kuwalinda wakulima” alisema Komba.
Naye Mkuu wa Wilaya Songea, Mhe. Pololet Mgema amewasisitiza wakulima watumie mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye kuuza mazao yao, kwani itawasaidia kuondokana wafanyabiashara wasio watakia mema.
“Mazao haya ambayo ni ya biashara kwa kiwango kidogo sisi tunayatumia na kwa kiasi kikubwa yanauzwa njee ya nchi, sasa tukiruhusu mazoa kama hayo yauzwe kiholela tutegemee mkulima atakuwa masikini na mwananchi akiona zao alimnufaishi anaacha kulima” alisema Mgema.
Wakulima wa halmashauri hiyo wanajihusisha na kulima mazoa wa biashara yakiwemo zao la Soya na Zao la ufuta.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.