UTAFITI wa kisanyansi unaonesha kuwa watu wanaokula samaki kwa wingi wakiwemo wakazi wa Mwambao mwa ziwa Nyasa wanakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, kutunza kumbukumbu na kuishi muda mrefu.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA ) Dk.Daniel Mushi ambaye amebobea katika Sayansi ya Nyama anasema samaki ambayo ni nyama nyeupe kama kuku, ni kitoweo Chenye mafuta aina ya Omega 3 yanayomfanya binadamu kuwa na akili nyingi na kutozeeka mapema.
Dr . Mushi anabainisha kuwa mafuta ya Omega 3 yaliopo kwenye samaki na nyama ya kuku yanazuia damu isigande kwenye mzunguko wa damu,pia yanaondoa madhara makubwa katika mwili,ndiyo maana baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani wametengeneza vidonge vya omega 3 kwa kutumia mafuta ya samaki.
Mwaka 2012 wanasanyansi wa Marekani walifanya utafiti kwa watu 17,478 wenye umri wa miaka 64 wanaoishi mwambao mwa bahari na maziwa na kubaini wamekuwa wakila samaki hivyo kuwa na uwezo wa kufikiri na kuishi muda mrefu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.