Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii pamoja na Makumbusho ya kihistoria.
Wito huo umetolewa na Afisa Elimu wa Makumbusho ya taifa ya Majimaji Rose Kangu wakati akiongea na Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM ) Kitivo cha Utalii na Utamaduni walipotembelea makumbusho hayo yaliyopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Kangu amesema kutembelea Makumbusho hayo ambayo yametumika kuhifadhi na kuonesha historia ya Vita vya Maji Maji vilivyotokea mwaka 1905 -1907, utumika kutoa elimu jinsi mababu zetu walivyopambana na Wakoloni ili kulinda Utu na heshma yetu wa Afrika
"Wadau wetu wakubwa wamekuwa ni wanafunzi wanaokuja kuitembelea Makumbusho hii, Ni kizazi ambacho tunakihitaji sana kurithisha Urithi huu kwa kizazi Kijacho, Kama tunavyojua sisi tunatunza historia adhimu ya hivyo niwaombe watanzania tujiweke utaribu wa kutembelea makumbuho”amesema.
Aidha, ametoa wito kwa wadau Mbalimbali kuitembelea Makumbusho hiyo kwani licha kupata Burudani wataweza jifunza historia adhimu ya Mashuja wa Vita hiyo iluyopiganwa Kwa muda mrefu zaidi Barani Afrika na faida za kuenzi Utamaduni wetu.
Kalebi Christopher mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM ) anayesoma Kitivo cha Utalii na Utamaduni amesema amevutiwa na historia ya vita vya majimaji pia amewashauri wanafunzi wenzake wa vyuo vingine pamoja na Shule za sekondari na msingi kwenda kutembelea Makumbusho hiyo kutokana na kuwepo kwa vitu vingi vya kujifunza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.