Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma inatarajia kutoa chanjo ya kuzuia Saratani ya shingo ya kizazi kwa Watoto wa kike 22,550 wenye umri wa miaka 9 hadi 14 .
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba kwenye uzinduzi wa kampeni ya chanjo hiyo uliofanyika katika shule ya msingi Chifu Songea Mbano iliyopo katika Kata ya Ruvuma mjini Songea.
Katika ufunguzi huo Watoto wa kike 204 wa shule hiyo walipatiwa chanjo hiyo.
Akizungumza kwenye kampeni hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka mabinti zao kupata chanjo hiyo ambayo imethibitika kitaalamu kuwa haina madhara yeyote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.