Watumishi wa umma 24 kutoka katika Ofisi ya Rais Utumishi Makao makuu Dodoma wamefanya utalii wa ndani katika bustani ya Wanyamapori Ruhila iliyopo mjini Songea mkoani Ruvuma.
Watumishi hao wametembelea bustani hiyo ya asili wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais Ndugu Mwanaamani Mtoo na kupokelewa na Kaimu Kamanda wa Kituo hicho kilichopo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) bwana Olekuney.
Watumishi hao walijionea vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye bustani hiyo wakiwemo Wanyamapori kama simba.pundamilia na nyumbu.
Wakizungumza baada ya kuona vivutio hivyo wamepongeza juhudi za TAWA za kuboresha utalii wa ndani hali inayovutia watalii wengi !
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.