WATUMISHI wa kada mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma,wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazo fanya kwa kuwajali na kuridhia nyongeza ya mshahara wa kima cha chini kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma.
Walisema,kuwathamini na ongezeko la mshahara na maboresho ya maslahi mbalimbali ya watumishi yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia yanakwenda kuchochea na kuongeza morali ya uwajibikaji kwa watumishi hao.
Wametoa pongezi hizo jana mbele ya Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro,walipokutana kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia kutokana na mafanikio yake katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wake.
Mdhibiti wa ubora wa shule wilaya ya Tunduru Halima Nyenje, amempongeza Rais Samia kwa uamuzi huo ambao utaleta ari ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma kwa kuwa wao ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi na wana mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa letu.
Aidha alisema, hatua ya kulipa malimbikizo,ongezeko la mishahara na maboresho yaliyofanywa na Rais Samia kwa watumishi wa umma ni ishara ya upendo wa serikali kwa watumishi wake na unapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote.
Mwalimu Nyenje, amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa wilaya hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali,ikiwamo fedha zilizoletwa kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ,miradi ya maji na sekta ya afya.
Blandina Sekela alisema kuwa,Rais Samia katika kipindi cha uongozi wake wa mwaka mmoja na miezi kadhaa ameweza kuleta nafuu na faraja kubwa kwa watumishi wa umma.Sekala ambaye ni afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya wilaya hiyo alisema,kutokana na nyongeza hiyo ya mishahara na maboresho mengine,wananchi wategemee kupata huduma bora.
Sekela ametolea mfano,katika idara ya afya wamepata watumishi wapya 53 ambao wamepelekwa katika maeneo mbalimbali ambao wamekwenda kuongezeka kwenye baadhi ya vituo ambavyo havikuwa na watumishi wa kutosha.
Alisema,watumishi hao watafanya kazi ya kuwahudumia wananchi kwa karibu zaidi hatua itakayowezesha sana kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuwa huduma hizo zitasogezwa karibu na wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Chiza Marando alisema,katika kipindi cha cha mwaka 2021/2022 jumla ya watumishi 139 wa kada tofauti wa Halmashauri hiyo wamepandishwa vyeo na Serikali,kulipa kiasi cha Sh.milioni 42,468,000 kila mwezi kutokana na upandishaji wa vyeo watumishi hao.
Alieleza kuwa, katika kipindi hicho watumishi 39 wa kada tofauti wamebadilishwa vyeo ili kukidhi mahitaji ya watumishi katika idara mbalimbali na Serikali inalipa Sh.milioni 12,612,000 kila mwezi zinazotokana na kubadilishwa kada watumishi hao.
Marando alisema,watumishi 94 wa idara mbalimbali katika Halmashauri hiyo wamelipwa Sh.milioni 85,728,280 kama malimbikizo pamoja na kuajiri watumishi 123 ambao wanalipwa Sh.milioni 82,902,000 kila mwezi.
Akizungumzia kuhusu nyongeza ya mishara iliyoanza mwezi julai mwaka huu Marando alisema,katika Halmshauri ya wilaya Tunduru mishahara imeongezeka kutoka Sh.milioni 829,973,075 hadi Sh.milioni 956,625,177.95 kwa mwezi na hivyo kufanya ongezeko la Sh. 126,652,101.95.
Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watumishi na kuwalipa maslahi yao na jambo lililosaidia sana watumishi kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza azma ya Serikali ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi wa Tunduru.
Akizungumzia juu ya sensa ya watu na makazi iliyoanza leo nchini kote Marando alisema,maandalizi yamekamilika kwa asilimia 98 na hadi sasa wamepokea Sh.bilioni 1.9 kati ya bilioni 2.662,000,000 zilizopangwa kutumika kwa ajili yakufanikisha sensa ya mwaka 2022.Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro alisema, nyongeza ya asilimia 23.ya mishahara kwa watumishi wa umma,Rais Samia amezingatia kuboresha hali ya kiuchumi za watumishi wa kiwango cha chini ambao ni wengi zaidi katika kada mbalimbali na wana viwango vidogo vya mishahara.
Alisema,Rais Samia amejipambanua kwa kuwajali watumishi wake na kuzingatia maslahi na alianza kwa kuwaondolea kadhia ya watumishi wenye deni la mkopo wa elimu ya juu na umeleta unafuu mkubwa wa maisha kwa watumishi hao.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya,katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wake,Rais Samia amepeleka zaidi ya Sh.bilioni 22 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii katika wilaya hiyo.
Amewataka watumishi idara na taasisi mbalimbali za serikali kumuunga mkono Rais Samia kwa kufanya kazi kwa bidii,kumpongeza,kumshukuru na kumuombea ili aweze kuishi maisha marefu na aendelee kutafuta fedha kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii hapa nchini.
MWISHOOOOOO.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.