Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa ameagiza kuondolewa kwa Mhandisi Mshauri LEA Associaties anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kitai - Lituhi sehemu ya Amani Makoro-Ruanda (km 35) kwa kiwango cha lami na kuutaka Wakala wa Barabara (TANROADS) kuendelea kusimamia ujenzi huo ili uweze kukamilika.
Bashungwa ametoa agizo hilo tarehe 25 Januari 2024 wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo ambapo hajaridhishwa na utekelezaji wake ambao umechelewa.
“Nimuagize Katibu Mkuu kuangalia hatua za kimkataba mnazotakiwa kumchukulia haraka Mhandisi Mshauri kwasababu ameshindwa kumsimamia Mkandarasi kukamilisha mradi huu kwa wakati”amesisitiza Waziri Bashungwa.
Amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishatoa Bilioni 6.9 ambayo imekamilisha kipande cha kwanza cha kilometa 5 kutoka Kitai hadi Amani Makoro na Bilioni 60 kwa ajili ya muendelezo wa barabara hiyo sehemu ya Amani Makoro - Ruanda.
Akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Jephason Nko, amesema kuwa maendeleo ya mradi huo mpaka sasa umefikia 25% ikilinganishwa na 100% ambapo mradi huo ulitakiwa kukamilika Disemba, 2023.
Akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Jephason Nko, amesema kuwa maendeleo ya mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 25 ikilinganishwa na asilimia 100 ambapo mradi huo ulitakiwa kukamilika Disemba, 2023.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma , Kanali Labani Thomas, amesema kuwa Mchuchuma na Liganga wanaitegemea barabara hii kwani ndio barabara muhimu na ni kiunganishi cha kutoka Mkoa wa Ruvuma kupitia Nyasa kwenda mkoani Njombe kupitia Ludewa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Mhe. Benaya kapinga, amesema kuwa kilio kikubwa cha Wananchi wa Amani - makoro hadi Ruanda ni kupata barabara kwa kiwango cha lami ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.