WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amezindua ofisi ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma katika hafla ambayo imefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watendaji kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma wakiwemo wakazi wa mji wa Songea,Waziri Lukuvi katika hafla hiyo pia aligawa hati miliki kwa baadhi ya wananchi.
Kabla ya kufunguliwa kwa ofisi hiyo wananchi wa Mkoa wa Ruvuma walikuwa wanasafiri umbali mrefu hadi mkoani Mtwara kufuatilia kusajili Hati zao ili kupata hatimiliki.
Akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo Waziri Lukuvi amesema wananchi watumie ofisi hiyo na wataalamu ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi iliyokuwa inajitokeza hapo mwanzo .
‘’Ofisi hii ni yenu wana Ruvuma na Wakurugenzi na mnatakiwa kuitumia ipasavyo tutaleta mitambo na kuskani majalada yenu yaliyotunzwa nyaraka mbalimbali za umilikishaji wa ardhi zote ili ziingie kwenye mfumo na ramani zote ziingie kwenye mfumo tunataka, masikini na tajiri wamilikishwe eneo na serikali ipate kodi’’,alisisitiza.
Lukuvi amesema mwananchi wa kawaida Hati yake ikisajiliwa kwenye ofisi ya Mkoa lazima serikali impelekee nakwamba hata wale wananchi vijijini hati zao zimepekwe kwenye halmashauri zao.
Amemwagiza Msajili wa Hati awalasimishe maafisa ardhi ili waweze kusajili hati hivyo kusababisha kila mwananchi kupata hati yake kwa wakati.
‘’Nimemwagiza msajili wa hati kwamba mwananchi wa kawaida hati yake ikishatoka Mbinga na imesajiliwa ofisi za Mkoa ni marufuku kwa mwananchi huyo kufuata hati achukua katika halmashauri yake, ardhi isiwe na usumbufu tena katika kupata hati’’,alisema Lukuvi.
Lukuvi pia ametoa onyo kwa wanasheria wanaowadanganya wananchi kuwafuatilia hati zao Mtwara ili wawatapeli hela zao kwa sababu mkoa wa Ruvuma hivi sasa unatoa huduma hizo na kwamba kuanzia mwananchi anapojaza fomu asilipe gharama yoyote.
Hata hivyo amesema katika uzinduzi huo amerudisha nyaraka zote zilizokuwepo Mtwara kabla na baada ya uhuru za mkoa wa Ruvuma za michoro na upimaji za kumbukumbu zote na kufanya uwezeshaji mwepesi.
Waziri huyo wa Ardhi amesema kupitia ofisi ya Ardhi ya Mkoa wa Ruvuma sasa wananchi wanaweza kukopesheka na kuongeza mzunguko wa pesa katika kilimo na kukopa benki.
Imeandikwa na Anet Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Agosti 11,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.